Native Bible

2 Samuel 23:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

yeye ni kama mwanga wa asubuhi jua lichomozapo asubuhi isiyo na mawingu, kama mwanga baada ya mvua uchipuzao majani kutoka ardhini.’

2 Samuel 23:4 in English

2 Samuel 23:4 · Berean Standard Bible

is like the light of the morning at sunrise of a cloudless dawn, the glistening after the rain on the sprouting grass of the earth.’

Context

2“Roho wa Bwana alinena kupitia kwangu, neno lake lilikuwa ulimini mwangu. 3Mungu wa Israeli alinena, mwamba wa Israeli akaniambia: ‘Mtu anatawala watu kwa haki, wakati anapotawala akiwa na hofu ya Mungu, 4yeye ni kama mwanga wa asubuhi jua lichomozapo asubuhi isiyo na mawingu, kama mwanga baada ya mvua uchipuzao majani kutoka ardhini.’ 5“Je, si hivyo ilivyo nyumba yangu mbele za Mungu? Je, hajafanya Agano la milele nami, lililopangwa na kuimarishwa kila sehemu? Je, hatanifanya niufurahie wokovu wangu na kunijalia matakwa yangu yote? 6Lakini watu waovu wote watatupwa kando kama miiba, ambayo haikusanywi kwa mkono.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.