2 Samweli 23:3
2 Samuel 23:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mungu wa Israeli alinena, mwamba wa Israeli akaniambia: ‘Mtu anatawala watu kwa haki, wakati anapotawala akiwa na hofu ya Mungu,
2 Samuel 23:3 in English
2 Samuel 23:3 · Berean Standard Bible
The God of Israel spoke; the Rock of Israel said to me, ‘He who rules the people with justice, who rules in the fear of God,
Context
1Haya ni maneno ya mwisho ya Daudi:
“Neno la Daudi mwana wa Yese,
neno la mtu aliyeinuliwa na Aliye Juu Sana,
mtu aliyepakwa mafuta na Mungu wa Yakobo,
mwimbaji wa nyimbo wa Israeli: 2“Roho wa Bwana alinena kupitia kwangu,
neno lake lilikuwa ulimini mwangu. 3Mungu wa Israeli alinena,
mwamba wa Israeli akaniambia:
‘Mtu anatawala watu kwa haki,
wakati anapotawala
akiwa na hofu ya Mungu, 4yeye ni kama mwanga wa asubuhi jua lichomozapo
asubuhi isiyo na mawingu,
kama mwanga baada ya mvua
uchipuzao majani kutoka ardhini.’ 5“Je, si hivyo ilivyo nyumba yangu
mbele za Mungu?
Je, hajafanya Agano la milele nami,
lililopangwa na kuimarishwa
kila sehemu?
Je, hatanifanya niufurahie wokovu wangu
na kunijalia matakwa yangu yote?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.