Native Bible

2 Samuel 23:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Roho wa Bwana alinena kupitia kwangu, neno lake lilikuwa ulimini mwangu.

2 Samuel 23:2 in English

2 Samuel 23:2 · Berean Standard Bible

The Spirit of the LORD spoke through me; His word was on my tongue.

Context

1Haya ni maneno ya mwisho ya Daudi: “Neno la Daudi mwana wa Yese, neno la mtu aliyeinuliwa na Aliye Juu Sana, mtu aliyepakwa mafuta na Mungu wa Yakobo, mwimbaji wa nyimbo wa Israeli: 2“Roho wa Bwana alinena kupitia kwangu, neno lake lilikuwa ulimini mwangu. 3Mungu wa Israeli alinena, mwamba wa Israeli akaniambia: ‘Mtu anatawala watu kwa haki, wakati anapotawala akiwa na hofu ya Mungu, 4yeye ni kama mwanga wa asubuhi jua lichomozapo asubuhi isiyo na mawingu, kama mwanga baada ya mvua uchipuzao majani kutoka ardhini.’

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.