Native Bible

2 Samuel 22:33 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu.

2 Samuel 22:33 in English

2 Samuel 22:33 · Berean Standard Bible

God is my strong fortress and He makes my way clear.

Context

31“Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu; neno la Bwana halina dosari. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake. 32Kwa maana ni nani aliye Mungu zaidi ya Bwana? Ni nani aliye Mwamba isipokuwa Mungu wetu? 33Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu. 34Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu, huniwezesha kusimama mahali palipo juu. 35Huifundisha mikono yangu kupigana vita; mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.