Native Bible

2 Samuel 22:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa maana ni nani aliye Mungu zaidi ya Bwana? Ni nani aliye Mwamba isipokuwa Mungu wetu?

2 Samuel 22:32 in English

2 Samuel 22:32 · Berean Standard Bible

For who is God besides the LORD? And who is the Rock except our God?

Context

30Kwa msaada wako naweza kushinda jeshi, nikiwa pamoja na Mungu wangu nitaweza kuruka ukuta. 31“Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu; neno la Bwana halina dosari. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake. 32Kwa maana ni nani aliye Mungu zaidi ya Bwana? Ni nani aliye Mwamba isipokuwa Mungu wetu? 33Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu. 34Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu, huniwezesha kusimama mahali palipo juu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.