1 Wathesalonike 5:10
1 Thessalonians 5:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yeye alikufa kwa ajili yetu ili hata kama tuko macho au tumelala, tupate kuishi pamoja naye.
1 Thessalonians 5:10 in English
1 Thessalonians 5:10 · Berean Standard Bible
He died for us so that, whether we are awake or asleep, we may live together with Him.
Context
8Lakini kwa kuwa sisi ni wana wa mchana, basi tuwe na kiasi, tukijivika imani na upendo kama dirii kifuani na tumaini letu la wokovu kama chapeo. 9Kwa maana Mungu hakutuita ili tupate ghadhabu bali tupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. 10Yeye alikufa kwa ajili yetu ili hata kama tuko macho au tumelala, tupate kuishi pamoja naye. 11Kwa hiyo farijianeni na kujengana, kama vile mnavyofanya sasa. 12Sasa tunawaomba, ndugu, waheshimuni wale wanaofanya kazi kwa bidii miongoni mwenu, wale ambao wana mamlaka juu yenu katika Bwana na ambao wanawaonya.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.