Native Bible

1 Samuel 17:56 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mfalme akasema, “Uliza huyu kijana ni mwana wa nani.”

1 Samuel 17:56 in English

1 Samuel 17:56 · Berean Standard Bible

“Find out whose son this young man is!” said the king.

Context

54Daudi akachukua kichwa cha yule Mfilisti na kukileta Yerusalemu, naye akaweka silaha za huyo Mfilisti katika hema lake mwenyewe. 55Sauli alipomwona Daudi anakwenda kukabiliana na huyo Mfilisti, alimwambia Abneri, jemadari wa jeshi, “Abneri, yule kijana ni mwana wa nani?” Abneri akajibu, “Hakika kama uishivyo, ee mfalme, mimi sifahamu.” 56Mfalme akasema, “Uliza huyu kijana ni mwana wa nani.” 57Mara Daudi aliporudi kutoka kumuua huyo Mfilisti, Abneri akamchukua na kumleta mbele ya Sauli. Daudi alikuwa bado anakishikilia kichwa cha yule Mfilisti. 58Sauli akamuuliza, “Kijana, wewe ni mwana wa nani?” Daudi akasema, “Mimi ni mwana wa mtumishi wako Yese wa Bethlehemu.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.