1 Nyakati 6:32
1 Chronicles 6:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Solomoni alipojenga Hekalu la Bwana huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.
1 Chronicles 6:32 in English
1 Chronicles 6:32 · Berean Standard Bible
They ministered with song before the tabernacle, the Tent of Meeting, until Solomon built the house of the LORD in Jerusalem. And they performed their duties according to the regulations given them.
Context
30Uza akamzaa Shimea, Shimea akamzaa Hagia,
Hagia akamzaa Asaya. 31Hawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya Bwana, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko. 32Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Solomoni alipojenga Hekalu la Bwana huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa. 33Wafuatao ni watu waliohudumu pamoja na wana wao:
Kutoka ukoo wa Kohathi walikuwa:
Hemani, mpiga kinanda,
alikuwa mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli, 34mwana wa Elikana, mwana wa Yerohamu,
mwana wa Elieli, mwana wa Toa,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.