Native Bible

1 Chronicles 6:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Uza akamzaa Shimea, Shimea akamzaa Hagia, Hagia akamzaa Asaya.

1 Chronicles 6:30 in English

1 Chronicles 6:30 · Berean Standard Bible

Shimea his son, Haggiah his son, and Asaiah his son.

Context

28Wana wa Samweli walikuwa: Yoeli mzaliwa wake wa kwanza, na Abiya mwanawe wa pili. 29Wafuatao ndio wazao wa Merari: Merari akamzaa Mahli, Mahli akamzaa Libni, Libni akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Uza, 30Uza akamzaa Shimea, Shimea akamzaa Hagia, Hagia akamzaa Asaya. 31Hawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya Bwana, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko. 32Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Solomoni alipojenga Hekalu la Bwana huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.