1 Nyakati 5:12
1 Chronicles 5:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yoeli ndiye alikuwa mkuu wao, Shafamu wa pili, na wakafuata Yanai na Shafati, huko Bashani.
1 Chronicles 5:12 in English
1 Chronicles 5:12 · Berean Standard Bible
Joel was the chief, Shapham the second, then Jaanai and Shaphat, who lived in Bashan.
Context
10Wakati wa utawala wa Mfalme Sauli, walipigana vita dhidi ya Wahagari, wakaanguka kwa mikono yao, kisha wakaishi katika mahema ya Wahagari katika eneo lote la mashariki ya Gileadi. 11Wagadi waliishi jirani nao katika nchi ya Bashani, mpaka Saleka. 12Yoeli ndiye alikuwa mkuu wao, Shafamu wa pili, na wakafuata Yanai na Shafati, huko Bashani. 13Ndugu zao kulingana na koo zao walikuwa saba:
Mikaeli, Meshulamu, Sheba, Yorai, Yakani, Zia na Eberi. 14Hawa walikuwa ndio wana wa Abihaili mwana wa Huri, mwana wa Yaroa, mwana wa Gileadi, mwana wa Mikaeli, mwana wa Yeshishai, mwana wa Yahdo, mwana wa Buzi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.