Native Bible

1 Chronicles 5:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wagadi waliishi jirani nao katika nchi ya Bashani, mpaka Saleka.

1 Chronicles 5:11 in English

1 Chronicles 5:11 · Berean Standard Bible

The descendants of Gad lived next to the Reubenites in the land of Bashan, as far as Salecah:

Context

9Kwa upande wa mashariki walienea hadi pembeni mwa jangwa linaloenea mpaka kwenye Mto Frati, kwa sababu mifugo yao ilikuwa imeongezeka huko Gileadi. 10Wakati wa utawala wa Mfalme Sauli, walipigana vita dhidi ya Wahagari, wakaanguka kwa mikono yao, kisha wakaishi katika mahema ya Wahagari katika eneo lote la mashariki ya Gileadi. 11Wagadi waliishi jirani nao katika nchi ya Bashani, mpaka Saleka. 12Yoeli ndiye alikuwa mkuu wao, Shafamu wa pili, na wakafuata Yanai na Shafati, huko Bashani. 13Ndugu zao kulingana na koo zao walikuwa saba: Mikaeli, Meshulamu, Sheba, Yorai, Yakani, Zia na Eberi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.