Native Bible

1 Chronicles 5:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa upande wa mashariki walienea hadi pembeni mwa jangwa linaloenea mpaka kwenye Mto Frati, kwa sababu mifugo yao ilikuwa imeongezeka huko Gileadi.

1 Chronicles 5:9 in English

1 Chronicles 5:9 · Berean Standard Bible

They also settled in the east as far as the edge of the desert that extends to the Euphrates River, because their livestock had increased in the land of Gilead.

Context

7Jamaa zao kulingana na koo zao, walioorodheshwa kwa kufuata koo zao kama ifuatavyo: Yeieli aliyekuwa mkuu wao, Zekaria, 8Bela mwana wa Azazi, mwana wa Shema, mwana wa Yoeli. Hao waliishi katika eneo kuanzia Aroeri mpaka Nebo na Baal-Meoni. 9Kwa upande wa mashariki walienea hadi pembeni mwa jangwa linaloenea mpaka kwenye Mto Frati, kwa sababu mifugo yao ilikuwa imeongezeka huko Gileadi. 10Wakati wa utawala wa Mfalme Sauli, walipigana vita dhidi ya Wahagari, wakaanguka kwa mikono yao, kisha wakaishi katika mahema ya Wahagari katika eneo lote la mashariki ya Gileadi. 11Wagadi waliishi jirani nao katika nchi ya Bashani, mpaka Saleka.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.