1 Nyakati 5:10
1 Chronicles 5:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakati wa utawala wa Mfalme Sauli, walipigana vita dhidi ya Wahagari, wakaanguka kwa mikono yao, kisha wakaishi katika mahema ya Wahagari katika eneo lote la mashariki ya Gileadi.
1 Chronicles 5:10 in English
1 Chronicles 5:10 · Berean Standard Bible
During the days of Saul they waged war against the Hagrites, who were defeated at their hands, and they occupied the homes of the Hagrites throughout the region east of Gilead.
Context
8Bela mwana wa Azazi, mwana wa Shema, mwana wa Yoeli. Hao waliishi katika eneo kuanzia Aroeri mpaka Nebo na Baal-Meoni. 9Kwa upande wa mashariki walienea hadi pembeni mwa jangwa linaloenea mpaka kwenye Mto Frati, kwa sababu mifugo yao ilikuwa imeongezeka huko Gileadi. 10Wakati wa utawala wa Mfalme Sauli, walipigana vita dhidi ya Wahagari, wakaanguka kwa mikono yao, kisha wakaishi katika mahema ya Wahagari katika eneo lote la mashariki ya Gileadi. 11Wagadi waliishi jirani nao katika nchi ya Bashani, mpaka Saleka. 12Yoeli ndiye alikuwa mkuu wao, Shafamu wa pili, na wakafuata Yanai na Shafati, huko Bashani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.