1 Nyakati 29:9
1 Chronicles 29:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watu wakafurahi kwa sababu ya itikio la hiari la viongozi wao, kwa kuwa walikuwa wametoa kwa hiari na kwa moyo wote kwa Bwana. Mfalme Daudi pia akafurahi sana.
1 Chronicles 29:9 in English
1 Chronicles 29:9 · Berean Standard Bible
And the people rejoiced at the willing response of their leaders, for they had given to the LORD freely and wholeheartedly. And King David also rejoiced greatly.
Context
7Wakatoa kwa ajili ya kazi ya Hekalu la Mungu talanta 5,000* na darkoni 10,000* za dhahabu, talanta 10,000* za fedha, talanta 18,000* za shaba na talanta 100,000* za chuma. 8Kila mmoja aliyekuwa na vito vya thamani akavitoa katika hazina ya Hekalu la Bwana chini ya uangalizi wa Yehieli Mgershoni. 9Watu wakafurahi kwa sababu ya itikio la hiari la viongozi wao, kwa kuwa walikuwa wametoa kwa hiari na kwa moyo wote kwa Bwana. Mfalme Daudi pia akafurahi sana. 10Daudi akamhimidi Bwana mbele ya kusanyiko lote, akisema:
“Uhimidiwe wewe, Ee Bwana,
Mungu wa Israeli baba yetu,
tangu milele hata milele. 11Ukuu na uweza, ni vyako, Ee Bwana,
na utukufu na enzi na uzuri,
kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani
ni chako wewe.
Ee Bwana, ufalme ni wako;
umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.