1 Nyakati 29:10
1 Chronicles 29:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Daudi akamhimidi Bwana mbele ya kusanyiko lote, akisema: “Uhimidiwe wewe, Ee Bwana, Mungu wa Israeli baba yetu, tangu milele hata milele.
1 Chronicles 29:10 in English
1 Chronicles 29:10 · Berean Standard Bible
Then David blessed the LORD in the sight of all the assembly and said: “May You be blessed, O LORD, God of our father Israel, from everlasting to everlasting.
Context
8Kila mmoja aliyekuwa na vito vya thamani akavitoa katika hazina ya Hekalu la Bwana chini ya uangalizi wa Yehieli Mgershoni. 9Watu wakafurahi kwa sababu ya itikio la hiari la viongozi wao, kwa kuwa walikuwa wametoa kwa hiari na kwa moyo wote kwa Bwana. Mfalme Daudi pia akafurahi sana. 10Daudi akamhimidi Bwana mbele ya kusanyiko lote, akisema:
“Uhimidiwe wewe, Ee Bwana,
Mungu wa Israeli baba yetu,
tangu milele hata milele. 11Ukuu na uweza, ni vyako, Ee Bwana,
na utukufu na enzi na uzuri,
kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani
ni chako wewe.
Ee Bwana, ufalme ni wako;
umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote. 12Utajiri na heshima vyatoka kwako;
wewe ndiwe utawalaye vitu vyote.
Mikononi mwako kuna nguvu na uweza
ili kuinua na kuwapa wote nguvu,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.