1 Nyakati 29:8
1 Chronicles 29:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kila mmoja aliyekuwa na vito vya thamani akavitoa katika hazina ya Hekalu la Bwana chini ya uangalizi wa Yehieli Mgershoni.
1 Chronicles 29:8 in English
1 Chronicles 29:8 · Berean Standard Bible
Whoever had precious stones gave them to the treasury of the house of the LORD, under the care of Jehiel * the Gershonite.
Context
6Ndipo viongozi wa jamaa, maafisa wa kabila za Israeli, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, pamoja na maafisa waliokuwa wasimamizi wa kazi za mfalme wakatoa kwa hiari yao. 7Wakatoa kwa ajili ya kazi ya Hekalu la Mungu talanta 5,000* na darkoni 10,000* za dhahabu, talanta 10,000* za fedha, talanta 18,000* za shaba na talanta 100,000* za chuma. 8Kila mmoja aliyekuwa na vito vya thamani akavitoa katika hazina ya Hekalu la Bwana chini ya uangalizi wa Yehieli Mgershoni. 9Watu wakafurahi kwa sababu ya itikio la hiari la viongozi wao, kwa kuwa walikuwa wametoa kwa hiari na kwa moyo wote kwa Bwana. Mfalme Daudi pia akafurahi sana. 10Daudi akamhimidi Bwana mbele ya kusanyiko lote, akisema:
“Uhimidiwe wewe, Ee Bwana,
Mungu wa Israeli baba yetu,
tangu milele hata milele.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.