Native Bible

1 Chronicles 29:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ndipo viongozi wa jamaa, maafisa wa kabila za Israeli, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, pamoja na maafisa waliokuwa wasimamizi wa kazi za mfalme wakatoa kwa hiari yao.

1 Chronicles 29:6 in English

1 Chronicles 29:6 · Berean Standard Bible

Then the leaders of the households, the officers of the tribes of Israel, the commanders of thousands and of hundreds, and the officials in charge of the king’s work gave willingly.

Context

4talanta 3,000* za dhahabu (dhahabu ya Ofiri) na talanta 7,000* za fedha safi iliyosafishwa, kwa ajili ya kufunika kuta za Hekalu, 5kwa kazi ya dhahabu na kazi ya fedha na kwa kazi yote itakayofanywa na mafundi. Basi, ni nani anayependa kujitoa kwa Bwana leo?” 6Ndipo viongozi wa jamaa, maafisa wa kabila za Israeli, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, pamoja na maafisa waliokuwa wasimamizi wa kazi za mfalme wakatoa kwa hiari yao. 7Wakatoa kwa ajili ya kazi ya Hekalu la Mungu talanta 5,000* na darkoni 10,000* za dhahabu, talanta 10,000* za fedha, talanta 18,000* za shaba na talanta 100,000* za chuma. 8Kila mmoja aliyekuwa na vito vya thamani akavitoa katika hazina ya Hekalu la Bwana chini ya uangalizi wa Yehieli Mgershoni.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.