1 Nyakati 29:4
1 Chronicles 29:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
talanta 3,000* za dhahabu (dhahabu ya Ofiri) na talanta 7,000* za fedha safi iliyosafishwa, kwa ajili ya kufunika kuta za Hekalu,
1 Chronicles 29:4 in English
1 Chronicles 29:4 · Berean Standard Bible
three thousand talents of gold * (the gold of Ophir) and seven thousand talents of refined silver,* to overlay the walls of the buildings,
Context
2Kwa uwezo wangu wote nimetenga mali kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu: dhahabu kwa kazi za dhahabu, fedha kwa ajili ya fedha, shaba kwa kazi za shaba, chuma kwa kazi za chuma na miti kwa kazi za miti, vivyo hivyo vito vya shohamu kwa ajili ya kutia kwenye vijalizo, almasi, mawe ya rangi mbalimbali, aina zote za vito vya thamani na marmar; yote haya kwa wingi mno. 3Zaidi ya hayo, kwa kujitolea kwangu kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu, sasa ninatoa hazina zangu mwenyewe za dhahabu na fedha kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu, zaidi ya mali niliyotoa kwa ajili ya Hekalu hili takatifu: 4talanta 3,000* za dhahabu (dhahabu ya Ofiri) na talanta 7,000* za fedha safi iliyosafishwa, kwa ajili ya kufunika kuta za Hekalu, 5kwa kazi ya dhahabu na kazi ya fedha na kwa kazi yote itakayofanywa na mafundi. Basi, ni nani anayependa kujitoa kwa Bwana leo?” 6Ndipo viongozi wa jamaa, maafisa wa kabila za Israeli, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, pamoja na maafisa waliokuwa wasimamizi wa kazi za mfalme wakatoa kwa hiari yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.