1 Nyakati 29:11
1 Chronicles 29:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ukuu na uweza, ni vyako, Ee Bwana, na utukufu na enzi na uzuri, kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani ni chako wewe. Ee Bwana, ufalme ni wako; umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote.
1 Chronicles 29:11 in English
1 Chronicles 29:11 · Berean Standard Bible
Yours, O LORD, is the greatness and the power and the glory and the splendor and the majesty, for everything in heaven and on earth belongs to You. Yours, O LORD, is the kingdom, and You are exalted as head over all.
Context
9Watu wakafurahi kwa sababu ya itikio la hiari la viongozi wao, kwa kuwa walikuwa wametoa kwa hiari na kwa moyo wote kwa Bwana. Mfalme Daudi pia akafurahi sana. 10Daudi akamhimidi Bwana mbele ya kusanyiko lote, akisema:
“Uhimidiwe wewe, Ee Bwana,
Mungu wa Israeli baba yetu,
tangu milele hata milele. 11Ukuu na uweza, ni vyako, Ee Bwana,
na utukufu na enzi na uzuri,
kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani
ni chako wewe.
Ee Bwana, ufalme ni wako;
umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote. 12Utajiri na heshima vyatoka kwako;
wewe ndiwe utawalaye vitu vyote.
Mikononi mwako kuna nguvu na uweza
ili kuinua na kuwapa wote nguvu, 13Sasa, Mungu wetu, tunakushukuru
na kulisifu Jina lako tukufu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.