1 Nyakati 23:3
1 Chronicles 23:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Walawi waliokuwa na umri wa miaka thelathini au zaidi walihesabiwa, nayo hesabu ya wanaume ilikuwa 38,000.
1 Chronicles 23:3 in English
1 Chronicles 23:3 · Berean Standard Bible
The Levites thirty years of age or older were counted, and the total number of men was 38,000.
Context
1Daudi alipokuwa mzee aliyeshiba siku, akamfanya Solomoni mwanawe kuwa mfalme juu ya Israeli. 2Pia akawakusanya pamoja viongozi wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi. 3Walawi waliokuwa na umri wa miaka thelathini au zaidi walihesabiwa, nayo hesabu ya wanaume ilikuwa 38,000. 4Daudi akasema, “Miongoni mwa hawa, 24,000 watasimamia kazi ya Hekalu la Bwana na 6,000 watakuwa maafisa na waamuzi, 5na 4,000 watakuwa mabawabu, na wengine 4,000 watamsifu Bwana kwa ala za uimbaji nilizotoa kwa ajili ya kusudi hilo.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.