Native Bible

1 Chronicles 23:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yahathi alikuwa wa kwanza na Ziza wa pili, lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; kwa hiyo walihesabiwa kama jamaa moja, wakapewa wajibu kwa pamoja.

1 Chronicles 23:11 in English

1 Chronicles 23:11 · Berean Standard Bible

Jahath was the first and Zizah was the second; but Jeush and Beriah did not have many sons, so they were counted as one family and received a single assignment.

Context

9Wana wa Shimei walikuwa watatu: Shelomothi,* Hazieli na Harani. Hawa watatu walikuwa viongozi wa jamaa za Ladani. 10Nao wana wa Shimei walikuwa wanne: Yahathi, Zina,* Yeushi na Beria. 11Yahathi alikuwa wa kwanza na Ziza wa pili, lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; kwa hiyo walihesabiwa kama jamaa moja, wakapewa wajibu kwa pamoja. 12Wana wa Kohathi walikuwa wanne: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. 13Wana wa Amramu walikuwa: Aroni na Mose. Aroni waliwekwa wakfu, yeye na wazao wake milele, wawe wakiweka wakfu vitu ambavyo ni vitakatifu mno, kutoa dhabihu mbele za Bwana, kuhudumu mbele zake na kutamka baraka katika Jina la Bwana milele.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.