Sefania 2:10
Zephaniah 2:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hiki ndicho watarudishiwa kwa ajili ya kiburi chao, kwa kutukana na kudhihaki watu wa Bwana Mwenye Nguvu Zote.
Zephaniah 2:10 in English
Zephaniah 2:10 · Berean Standard Bible
This they shall have in return for their pride, for taunting and mocking the people of the LORD of Hosts.
Context
8“Nimeyasikia matukano ya Moabu
nazo dhihaka za Waamoni,
ambao waliwatukana watu wangu
na kutoa vitisho dhidi ya nchi yao. 9Hakika, kama niishivyo,”
asema Bwana Mwenye Nguvu Zote,
Mungu wa Israeli,
“hakika Moabu itakuwa kama Sodoma,
Waamoni kama Gomora:
mahali pa magugu na mashimo ya chumvi,
nchi ya ukiwa milele.
Mabaki ya watu wangu watawateka nyara;
mabaki ya taifa langu watarithi nchi yao.” 10Hiki ndicho watarudishiwa kwa ajili ya kiburi chao,
kwa kutukana na kudhihaki
watu wa Bwana Mwenye Nguvu Zote. 11Bwana atakuwa wa kuhofisha kwao
atakapoangamiza miungu yote ya nchi.
Mataifa katika kila pwani yatamwabudu,
kila moja katika nchi yake. 12“Ninyi pia, ee Wakushi,
mtauawa kwa upanga wangu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.