Native Bible

Zechariah 9:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wageni watakalia mji wa Ashdodi, nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti.

Zechariah 9:6 in English

Zechariah 9:6 · Berean Standard Bible

A mixed race will occupy Ashdod, and I will cut off the pride of the Philistines.

Context

4Lakini Bwana atamwondolea mali zake na kuuangamiza uwezo wake wa baharini, naye atateketezwa kwa moto. 5Ashkeloni ataona hili na kuogopa; Gaza atagaagaa kwa maumivu makali, pia Ekroni, kwa sababu matumaini yake yatanyauka. Gaza atampoteza mfalme wake na Ashkeloni ataachwa pweke. 6Wageni watakalia mji wa Ashdodi, nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti. 7Nitaondoa damu vinywani mwao, chakula kile walichokatazwa kati ya meno yao. Mabaki yao yatakuwa mali ya Mungu wetu, nao watakuwa viongozi katika Yuda, naye Ekroni atakuwa kama Wayebusi. 8Lakini nitailinda nyumba yangu dhidi ya majeshi ya wanyangʼanyi. Kamwe mdhalimu hatashambulia watu wangu tena, kwa maana sasa ninawachunga.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.