Zekaria 9:5
Zechariah 9:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ashkeloni ataona hili na kuogopa; Gaza atagaagaa kwa maumivu makali, pia Ekroni, kwa sababu matumaini yake yatanyauka. Gaza atampoteza mfalme wake na Ashkeloni ataachwa pweke.
Zechariah 9:5 in English
Zechariah 9:5 · Berean Standard Bible
Ashkelon will see and fear; Gaza will writhe in agony, as will Ekron, for her hope will wither. There will cease to be a king in Gaza, and Ashkelon will be uninhabited.
Context
3Tiro amejijengea ngome imara,
amelundika fedha kama mavumbi
na dhahabu kama taka za mitaani. 4Lakini Bwana atamwondolea mali zake
na kuuangamiza uwezo wake wa baharini,
naye atateketezwa kwa moto. 5Ashkeloni ataona hili na kuogopa;
Gaza atagaagaa kwa maumivu makali,
pia Ekroni, kwa sababu
matumaini yake yatanyauka.
Gaza atampoteza mfalme wake
na Ashkeloni ataachwa pweke. 6Wageni watakalia mji wa Ashdodi,
nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti. 7Nitaondoa damu vinywani mwao,
chakula kile walichokatazwa kati ya meno yao.
Mabaki yao yatakuwa mali ya Mungu wetu,
nao watakuwa viongozi katika Yuda,
naye Ekroni atakuwa kama Wayebusi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.