Zekaria 11:3
Zechariah 11:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sikiliza yowe la wachungaji; malisho yao manono yameangamizwa! Sikia ngurumo za simba; kichaka kilichostawi sana cha Yordani kimeharibiwa!
Zechariah 11:3 in English
Zechariah 11:3 · Berean Standard Bible
Listen to the wailing of the shepherds, for their glory is in ruins. Listen to the roaring of the young lions, for the thickets of the Jordan are destroyed.
Context
1Fungua milango yako, ee Lebanoni,
ili moto uteketeze mierezi yako! 2Piga yowe, ee mti wa msunobari,
kwa kuwa mwerezi umeanguka;
miti ya fahari imeharibiwa!
Piga yowe, enyi mialoni ya Bashani,
msitu mnene umefyekwa! 3Sikiliza yowe la wachungaji;
malisho yao manono yameangamizwa!
Sikia ngurumo za simba;
kichaka kilichostawi sana
cha Yordani kimeharibiwa! 4Hili ndilo asemalo Bwana Mungu wangu: “Lilishe kundi lililokusudiwa kuchinjwa. 5Wanunuzi wake huwachinja na kuondoka pasipo kuadhibiwa. Wale wanaowauza husema, ‘Bwana asifiwe, mimi ni tajiri!’ Wachungaji wao wenyewe hawawahurumii.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.