Wimbo 4:14
Song of Songs 4:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
nardo na zafarani, mchai na mdalasini, pamoja na kila aina ya mti wa uvumba, manemane na udi, na aina zote za vikolezo bora kuliko vyote.
Song of Songs 4:14 in English
Song of Songs 4:14 · Berean Standard Bible
with nard and saffron, with calamus and cinnamon, with every kind of frankincense tree, with myrrh and aloes, with all the finest spices.
Context
12Wewe ni bustani iliyofungwa, dada yangu,
bibi arusi wangu;
wewe ni chanzo cha maji kilichozungushiwa kabisa,
chemchemi yangu peke yangu. 13Mimea yako ni bustani ya mikomamanga
yenye matunda mazuri sana,
yenye hina na nardo, 14nardo na zafarani,
mchai na mdalasini,
pamoja na kila aina ya mti wa uvumba,
manemane na udi,
na aina zote za vikolezo bora kuliko vyote. 15Wewe ni chemchemi ya bustani,
kisima cha maji yatiririkayo,
yakitiririka kutoka Lebanoni. 16Amka, upepo wa kaskazini,
na uje, upepo wa kusini!
Vuma juu ya bustani yangu,
ili harufu yake nzuri iweze kuenea mpaka ngʼambo.
Mpendwa wangu na aje bustanini mwake
na kuonja matunda mazuri sana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.