Native Bible

Song of Songs 4:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wewe ni bustani iliyofungwa, dada yangu, bibi arusi wangu; wewe ni chanzo cha maji kilichozungushiwa kabisa, chemchemi yangu peke yangu.

Song of Songs 4:12 in English

Song of Songs 4:12 · Berean Standard Bible

My sister, my bride, you are a garden locked up, a spring enclosed, a fountain sealed.

Context

10Tazama jinsi pendo lako linavyofurahisha, dada yangu, bibi arusi wangu! Pendo lako linafurahisha aje zaidi ya divai, na harufu ya manukato yako zaidi ya kikolezo chochote! 11Midomo yako inadondosha utamu kama sega la asali, bibi arusi wangu; maziwa na asali viko chini ya ulimi wako. Harufu nzuri ya mavazi yako ni kama ile ya Lebanoni. 12Wewe ni bustani iliyofungwa, dada yangu, bibi arusi wangu; wewe ni chanzo cha maji kilichozungushiwa kabisa, chemchemi yangu peke yangu. 13Mimea yako ni bustani ya mikomamanga yenye matunda mazuri sana, yenye hina na nardo, 14nardo na zafarani, mchai na mdalasini, pamoja na kila aina ya mti wa uvumba, manemane na udi, na aina zote za vikolezo bora kuliko vyote.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.