Wimbo 4:11
Song of Songs 4:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Midomo yako inadondosha utamu kama sega la asali, bibi arusi wangu; maziwa na asali viko chini ya ulimi wako. Harufu nzuri ya mavazi yako ni kama ile ya Lebanoni.
Song of Songs 4:11 in English
Song of Songs 4:11 · Berean Standard Bible
Your lips, my bride, drip sweetness like the honeycomb; honey and milk are under your tongue, and the fragrance of your garments is like the aroma of Lebanon.
Context
9Umeiba moyo wangu, dada yangu, bibi arusi wangu;
umeiba moyo wangu
kwa mtazamo mmoja wa macho yako,
kwa kito kimoja cha mkufu wako. 10Tazama jinsi pendo lako linavyofurahisha,
dada yangu, bibi arusi wangu!
Pendo lako linafurahisha aje zaidi ya divai,
na harufu ya manukato yako zaidi ya kikolezo chochote! 11Midomo yako inadondosha utamu kama sega la asali,
bibi arusi wangu;
maziwa na asali viko chini ya ulimi wako.
Harufu nzuri ya mavazi yako ni kama ile ya Lebanoni. 12Wewe ni bustani iliyofungwa, dada yangu,
bibi arusi wangu;
wewe ni chanzo cha maji kilichozungushiwa kabisa,
chemchemi yangu peke yangu. 13Mimea yako ni bustani ya mikomamanga
yenye matunda mazuri sana,
yenye hina na nardo,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.