Native Bible

Song of Songs 3:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mfalme Solomoni alijitengenezea gari; alilitengeneza kwa mbao kutoka Lebanoni.

Song of Songs 3:9 in English

Song of Songs 3:9 · Berean Standard Bible

King Solomon has made his carriage out of the timber of Lebanon.

Context

7Tazama! Ni gari la Solomoni lisindikizwalo na mashujaa sitini, walio wakuu sana wa Israeli, 8wote wamevaa panga, wote wazoefu katika vita, kila mmoja na upanga wake pajani, wamejiandaa kwa ajili ya hofu za usiku. 9Mfalme Solomoni alijitengenezea gari; alilitengeneza kwa mbao kutoka Lebanoni. 10Nguzo zake alizitengeneza kwa fedha, kitako chake kwa dhahabu. Kiti chake kilipambwa kwa zambarau, gari lake likanakshiwa njumu kwa upendo na binti za Yerusalemu. 11Tokeni nje, ninyi binti za Sayuni, mkamtazame Mfalme Solomoni akiwa amevaa taji, taji ambalo mama yake alimvika siku ya arusi yake, siku ambayo moyo wake ulishangilia.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.