Native Bible

Song of Songs 2:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nitie nguvu kwa zabibu kavu, niburudishe kwa matofaa, kwa maana ninazimia kwa mapenzi.

Song of Songs 2:5 in English

Song of Songs 2:5 · Berean Standard Bible

Sustain me with raisins; refresh me with apples, for I am faint with love.

Context

3Kama mti wa mtofaa miongoni mwa miti ya msituni ndivyo alivyo mpenzi wangu miongoni mwa wanaume vijana. Ninafurahia kuketi kivulini mwa mwanaume huyu, na tunda lake ni tamu kwangu. 4Amenichukua mpaka kwenye ukumbi wa karamu, na bendera ya huyu mwanaume juu yangu ni upendo. 5Nitie nguvu kwa zabibu kavu, niburudishe kwa matofaa, kwa maana ninazimia kwa mapenzi. 6Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu, na mkono wake wa kuume unanikumbatia. 7Binti za Yerusalemu, ninawaagiza kwa paa na kwa ayala wa shambani: Msichochee wala kuamsha mapenzi hata yatakapotaka yenyewe.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.