Warumi 11:8
Romans 11:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
kama ilivyoandikwa: “Mungu aliwapa bumbuazi la mioyo, macho ili wasiweze kuona, na masikio ili wasiweze kusikia, hadi leo.”
Romans 11:8 in English
Romans 11:8 · Berean Standard Bible
as it is written: “God gave them a spirit of stupor, eyes that could not see, and ears that could not hear, to this very day.”*
Context
6Lakini ikiwa wamechaguliwa kwa neema, si tena kwa msingi wa matendo. Kama ingekuwa kwa matendo, neema isingekuwa neema tena. 7Tuseme nini basi? Kile kitu ambacho Israeli alikitafuta kwa bidii hakukipata. Lakini waliochaguliwa walikipata. Waliobaki walifanywa wagumu, 8kama ilivyoandikwa:
“Mungu aliwapa bumbuazi la mioyo,
macho ili wasiweze kuona,
na masikio ili wasiweze kusikia,
hadi leo.” 9Naye Daudi anasema:
“Karamu zao na ziwe tanzi na mtego wa kuwanasa,
kitu cha kuwakwaza waanguke, na adhabu kwao. 10Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona,
nayo migongo yao iinamishwe daima.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.