Warumi 11:10
Romans 11:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona, nayo migongo yao iinamishwe daima.”
Romans 11:10 in English
Romans 11:10 · Berean Standard Bible
May their eyes be darkened so they cannot see, and their backs be bent forever.”*
Context
8kama ilivyoandikwa:
“Mungu aliwapa bumbuazi la mioyo,
macho ili wasiweze kuona,
na masikio ili wasiweze kusikia,
hadi leo.” 9Naye Daudi anasema:
“Karamu zao na ziwe tanzi na mtego wa kuwanasa,
kitu cha kuwakwaza waanguke, na adhabu kwao. 10Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona,
nayo migongo yao iinamishwe daima.” 11Hivyo nauliza tena: Je, Waisraeli walijikwaa ili waanguke na kuangamia kabisa? La, hasha! Lakini kwa sababu ya makosa yao, wokovu umewafikia watu wa Mataifa, ili kuwafanya Waisraeli waone wivu. 12Basi ikiwa kukosa kwao kumekuwa utajiri mkubwa kwa ulimwengu, tena kama kuangamia kwao kumeleta utajiri kwa watu wa Mataifa, kurudishwa kwao kutaleta utajiri mkuu zaidi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.