Warumi 11:12
Romans 11:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi ikiwa kukosa kwao kumekuwa utajiri mkubwa kwa ulimwengu, tena kama kuangamia kwao kumeleta utajiri kwa watu wa Mataifa, kurudishwa kwao kutaleta utajiri mkuu zaidi.
Romans 11:12 in English
Romans 11:12 · Berean Standard Bible
But if their trespass means riches for the world, and their failure means riches for the Gentiles, how much greater riches will their fullness bring!
Context
10Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona,
nayo migongo yao iinamishwe daima.” 11Hivyo nauliza tena: Je, Waisraeli walijikwaa ili waanguke na kuangamia kabisa? La, hasha! Lakini kwa sababu ya makosa yao, wokovu umewafikia watu wa Mataifa, ili kuwafanya Waisraeli waone wivu. 12Basi ikiwa kukosa kwao kumekuwa utajiri mkubwa kwa ulimwengu, tena kama kuangamia kwao kumeleta utajiri kwa watu wa Mataifa, kurudishwa kwao kutaleta utajiri mkuu zaidi. 13Sasa ninasema nanyi watu wa Mataifa. Maadamu mimi ni mtume kwa watu wa Mataifa, naitukuza huduma yangu 14ili kuwafanya watu wangu waone wivu na hivyo kuwaokoa baadhi yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.