Warumi 10:18
Romans 10:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini nauliza: Je, wao hawakusikia? Naam, wamesikia, kwa maana: “Sauti yao imeenea duniani pote, nayo maneno yao yameenea hadi miisho ya ulimwengu.”
Romans 10:18 in English
Romans 10:18 · Berean Standard Bible
But I ask, did they not hear? Indeed they did: “Their voice has gone out into all the earth, their words to the ends of the world.”*
Context
16Lakini si wote waliotii Habari Njema. Kwa maana Isaya asema, “Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?” 17Basi, imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo. 18Lakini nauliza: Je, wao hawakusikia? Naam, wamesikia, kwa maana:
“Sauti yao imeenea duniani pote,
nayo maneno yao yameenea
hadi miisho ya ulimwengu.” 19Nami nauliza tena: Je, Waisraeli hawakuelewa? Kwanza, Mose asema,
“Nitawafanya mwe na wivu
kwa watu wale ambao si taifa.
Nitawakasirisha kwa taifa
lile lisilo na ufahamu.” 20Naye Isaya kwa ujasiri mwingi anasema,
“Nimeonekana na watu wale ambao hawakunitafuta.
Nilijifunua kwa watu
wale ambao hawakunitafuta.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.