Ufunuo 18:10
Revelation 18:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hofu kubwa ya mateso yake, watasimama mbali na kulia na wakisema: “ ‘Ole! Ole, ee mji mkubwa, ee Babeli mji wenye nguvu! Hukumu yako imekuja katika saa moja!’
Revelation 18:10 in English
Revelation 18:10 · Berean Standard Bible
In fear of her torment, they will stand at a distance and cry out: “Woe, woe to the great city, the mighty city of Babylon! For in a single hour your judgment has come.”
Context
8Kwa hiyo mapigo yatampata kwa siku moja:
mauti, maombolezo na njaa.
Naye atateketezwa kwa moto,
kwa maana Bwana Mungu amhukumuye ana nguvu. 9“Wafalme wa dunia waliozini naye na kushiriki anasa zake watakapoona moshi wa kuungua kwake, watamlilia na kumwombolezea. 10Kwa hofu kubwa ya mateso yake, watasimama mbali na kulia na wakisema:
“ ‘Ole! Ole, ee mji mkubwa,
ee Babeli mji wenye nguvu!
Hukumu yako imekuja katika saa moja!’ 11“Wafanyabiashara wa dunia watalia na kumwomboleza kwa sababu hakuna anunuaye bidhaa zao tena: 12Bidhaa za dhahabu, za fedha, za vito vya thamani na vya lulu, kitani safi, nguo za rangi ya zambarau, hariri, nguo nyekundu, aina zote za miti ya udi, na vifaa vyote vya pembe za ndovu, vifaa vyote vya miti yenye thamani kuliko yote, shaba, chuma na marmar,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.