Ufunuo 18:8
Revelation 18:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo mapigo yatampata kwa siku moja: mauti, maombolezo na njaa. Naye atateketezwa kwa moto, kwa maana Bwana Mungu amhukumuye ana nguvu.
Revelation 18:8 in English
Revelation 18:8 · Berean Standard Bible
Therefore her plagues will come in one day— death and grief and famine— and she will be consumed by fire, for mighty is the Lord God who judges her.”
Context
6Mtendee kama yeye alivyotenda;
umlipe mara mbili kwa ajili ya yale aliyotenda.
Katika kikombe chake mchanganyie
mara mbili ya kile alichochanganya. 7Mpatie mateso na huzuni nyingi sawa na
utukufu na anasa alizojipatia.
Kwa kuwa moyoni mwake hujivuna, akisema,
‘Mimi ninatawala kama malkia;
mimi si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.’ 8Kwa hiyo mapigo yatampata kwa siku moja:
mauti, maombolezo na njaa.
Naye atateketezwa kwa moto,
kwa maana Bwana Mungu amhukumuye ana nguvu. 9“Wafalme wa dunia waliozini naye na kushiriki anasa zake watakapoona moshi wa kuungua kwake, watamlilia na kumwombolezea. 10Kwa hofu kubwa ya mateso yake, watasimama mbali na kulia na wakisema:
“ ‘Ole! Ole, ee mji mkubwa,
ee Babeli mji wenye nguvu!
Hukumu yako imekuja katika saa moja!’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.