Native Bible

Revelation 18:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Wafalme wa dunia waliozini naye na kushiriki anasa zake watakapoona moshi wa kuungua kwake, watamlilia na kumwombolezea.

Revelation 18:9 in English

Revelation 18:9 · Berean Standard Bible

Then the kings of the earth who committed sexual immorality and lived in luxury with her will weep and wail at the sight of the smoke rising from the fire that consumes her.*

Context

7Mpatie mateso na huzuni nyingi sawa na utukufu na anasa alizojipatia. Kwa kuwa moyoni mwake hujivuna, akisema, ‘Mimi ninatawala kama malkia; mimi si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.’ 8Kwa hiyo mapigo yatampata kwa siku moja: mauti, maombolezo na njaa. Naye atateketezwa kwa moto, kwa maana Bwana Mungu amhukumuye ana nguvu. 9“Wafalme wa dunia waliozini naye na kushiriki anasa zake watakapoona moshi wa kuungua kwake, watamlilia na kumwombolezea. 10Kwa hofu kubwa ya mateso yake, watasimama mbali na kulia na wakisema: “ ‘Ole! Ole, ee mji mkubwa, ee Babeli mji wenye nguvu! Hukumu yako imekuja katika saa moja!’ 11“Wafanyabiashara wa dunia watalia na kumwomboleza kwa sababu hakuna anunuaye bidhaa zao tena:

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.