Native Bible

Psalms 91:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nitasema kumhusu Bwana, “Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu, ambaye ninamtumaini.”

Psalms 91:2 in English

Psalms 91:2 · Berean Standard Bible

I will say to the LORD, “You are my refuge and my fortress, my God, in whom I trust.”

Context

1Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana, atadumu katika uvuli wake Mwenyezi.* 2Nitasema kumhusu Bwana, “Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu, ambaye ninamtumaini.” 3Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji, na maradhi ya kuambukiza ya kuua. 4Atakufunika kwa manyoya yake, chini ya mbawa zake utapata kimbilio, uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.