Native Bible

Psalms 91:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji, na maradhi ya kuambukiza ya kuua.

Psalms 91:3 in English

Psalms 91:3 · Berean Standard Bible

Surely He will deliver you from the snare of the fowler, and from the deadly plague.

Context

1Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana, atadumu katika uvuli wake Mwenyezi.* 2Nitasema kumhusu Bwana, “Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu, ambaye ninamtumaini.” 3Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji, na maradhi ya kuambukiza ya kuua. 4Atakufunika kwa manyoya yake, chini ya mbawa zake utapata kimbilio, uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako. 5Hutaogopa vitisho vya usiku, wala mshale urukao mchana,

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.