Zaburi 90:12
Psalms 90:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri, ili tujipatie moyo wa hekima.
Psalms 90:12 in English
Psalms 90:12 · Berean Standard Bible
So teach us to number our days, that we may present a heart of wisdom.
Context
10Siku zetu za kuishi ni miaka sabini,
au miaka themanini ikiwa tuna nguvu,
lakini yote ni ya shida na taabu,
nazo zapita haraka, nasi twatoweka. 11Ni nani ajuaye nguvu za hasira yako?
Kwa maana ghadhabu yako ni kubwa
kama hofu tunayopaswa kuwa nayo kwako. 12Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri,
ili tujipatie moyo wa hekima. 13Ee Bwana, uwe na huruma! Utakawia hata lini?
Wahurumie watumishi wako. 14Tushibishe asubuhi kwa upendo wako usiokoma,
ili tuweze kuimba kwa shangwe na kufurahi siku zetu zote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.