Zaburi 90:10
Psalms 90:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Siku zetu za kuishi ni miaka sabini, au miaka themanini ikiwa tuna nguvu, lakini yote ni ya shida na taabu, nazo zapita haraka, nasi twatoweka.
Psalms 90:10 in English
Psalms 90:10 · Berean Standard Bible
The length of our days is seventy years— or eighty if we are strong— yet their pride is but labor and sorrow, for they quickly pass, and we fly away.
Context
8Umeyaweka maovu yetu mbele yako,
dhambi zetu za siri katika nuru ya uwepo wako. 9Tumeishi siku zetu zote chini ya ghadhabu yako,
tunamaliza miaka yetu kwa kuomboleza. 10Siku zetu za kuishi ni miaka sabini,
au miaka themanini ikiwa tuna nguvu,
lakini yote ni ya shida na taabu,
nazo zapita haraka, nasi twatoweka. 11Ni nani ajuaye nguvu za hasira yako?
Kwa maana ghadhabu yako ni kubwa
kama hofu tunayopaswa kuwa nayo kwako. 12Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri,
ili tujipatie moyo wa hekima.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.