Zaburi 9:12
Psalms 9:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana yeye alipizaye kisasi cha damu hukumbuka, hapuuzi kilio cha wanaoonewa.
Psalms 9:12 in English
Psalms 9:12 · Berean Standard Bible
For the Avenger of bloodshed remembers; He does not ignore the cry of the afflicted.
Context
10Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe,
kwa maana wewe Bwana,
hujawaacha kamwe wakutafutao. 11Mwimbieni Bwana sifa, amefanywa mtawala Sayuni,
tangazeni miongoni mwa mataifa, yale aliyoyatenda. 12Kwa maana yeye alipizaye kisasi cha damu hukumbuka,
hapuuzi kilio cha wanaoonewa. 13Ee Bwana, tazama jinsi walivyo wengi adui zangu wanaonitesa!
Nihurumie, uniinue kutoka malango ya mauti, 14ili niweze kutangaza sifa zako
katika malango ya Binti Sayuni
na huko niushangilie wokovu wako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.