Native Bible

Psalms 89:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Uliumba kaskazini na kusini; Tabori na Hermoni wanaliimbia jina lako kwa furaha.

Psalms 89:12 in English

Psalms 89:12 · Berean Standard Bible

North and south You created; Tabor and Hermon shout for joy at Your name.

Context

10Wewe ulimponda Rahabu* kama mmojawapo wa waliochinjwa; kwa mkono wako wenye nguvu, uliwatawanya adui zako. 11Mbingu ni zako, nayo nchi pia ni yako, uliuwekea ulimwengu msingi pamoja na vyote vilivyomo. 12Uliumba kaskazini na kusini; Tabori na Hermoni wanaliimbia jina lako kwa furaha. 13Mkono wako umejaa uwezo; mkono wako una nguvu, mkono wako wa kuume umetukuzwa. 14Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako cha enzi; upendo na uaminifu vinakutangulia.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.