Native Bible

Psalms 89:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mbingu ni zako, nayo nchi pia ni yako, uliuwekea ulimwengu msingi pamoja na vyote vilivyomo.

Psalms 89:11 in English

Psalms 89:11 · Berean Standard Bible

The heavens are Yours, and also the earth. The earth and its fullness You founded.

Context

9Wewe unatawala bahari yenye msukosuko; wakati mawimbi yake yanapoinuka, wewe unayatuliza. 10Wewe ulimponda Rahabu* kama mmojawapo wa waliochinjwa; kwa mkono wako wenye nguvu, uliwatawanya adui zako. 11Mbingu ni zako, nayo nchi pia ni yako, uliuwekea ulimwengu msingi pamoja na vyote vilivyomo. 12Uliumba kaskazini na kusini; Tabori na Hermoni wanaliimbia jina lako kwa furaha. 13Mkono wako umejaa uwezo; mkono wako una nguvu, mkono wako wa kuume umetukuzwa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.