Zaburi 88:3
Psalms 88:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana nafsi yangu imejaa taabu, na maisha yangu yanakaribia kaburi.*
Psalms 88:3 in English
Psalms 88:3 · Berean Standard Bible
For my soul is full of troubles, and my life draws near to Sheol.
Context
1Ee Bwana, Mungu uniokoaye,
nimelia mbele zako usiku na mchana. 2Maombi yangu yafike mbele zako,
utegee kilio changu sikio lako. 3Kwa maana nafsi yangu imejaa taabu,
na maisha yangu yanakaribia kaburi.* 4Nimehesabiwa miongoni mwa wale waendao shimoni,
niko kama mtu asiye na nguvu. 5Nimetengwa pamoja na wafu,
kama waliochinjwa walalao kaburini,
ambao huwakumbuki tena,
ambao wamekatiliwa mbali na uangalizi wako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.