Native Bible

Psalms 88:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Je, wewe huwaonyesha wafu maajabu yako? Je, wale waliokufa huinuka na kukusifu?

Psalms 88:10 in English

Psalms 88:10 · Berean Standard Bible

Do You work wonders for the dead? Do departed spirits rise up to praise You? Selah

Context

8Umenitenga na rafiki zangu wa karibu na kunifanya chukizo kwao. Nimezuiliwa, wala siwezi kutoroka; 9nuru ya macho yangu imefifia kwa ajili ya huzuni. Ee Bwana, ninakuita kila siku, ninakunyooshea wewe mikono yangu. 10Je, wewe huwaonyesha wafu maajabu yako? Je, wale waliokufa huinuka na kukusifu? 11Je, upendo wako hutangazwa kaburini, uaminifu wako katika Uharibifu?* 12Je, maajabu yako hujulikana mahali pa giza, au matendo yako ya haki katika nchi ya usahaulifu?

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.