Zaburi 80:14
Psalms 80:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Turudie, Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote! Tazama chini kutoka mbinguni na uone! Linda mzabibu huu,
Psalms 80:14 in English
Psalms 80:14 · Berean Standard Bible
Return, O God of Hosts, we pray! Look down from heaven and see! Attend to this vine—
Context
12Mbona umebomoa kuta zake
ili wote wapitao karibu
wazichume zabibu zake? 13Nguruwe mwitu wanauharibu
na wanyama wa kondeni hujilisha humo. 14Turudie, Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote!
Tazama chini kutoka mbinguni na uone!
Linda mzabibu huu, 15mche ulioupanda kwa mkono wako wa kuume,
mwana uliyemlea
kwa ajili yako mwenyewe. 16Mzabibu wako umekatwa, umechomwa moto,
unapowakemea, watu wako huangamia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.