Native Bible

Psalms 78:50 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Aliitengenezea njia hasira yake, hakuwaepusha na kifo, bali aliwaachia tauni.

Psalms 78:50 in English

Psalms 78:50 · Berean Standard Bible

He cleared a path for His anger; He did not spare them from death but delivered their lives to the plague.

Context

48Aliwaachia mifugo yao mvua ya mawe, akayapiga makundi ya wanyama wao kwa radi. 49Aliwafungulia hasira yake kali, ghadhabu yake, hasira na uadui, na kundi la malaika wa kuharibu. 50Aliitengenezea njia hasira yake, hakuwaepusha na kifo, bali aliwaachia tauni. 51Aliwapiga wazaliwa wote wa kwanza wa Misri, matunda ya kwanza ya ujana katika mahema ya Hamu. 52Lakini aliwatoa watu wake kama kundi, akawaongoza kama kondoo kupitia jangwani.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.