Native Bible

Psalms 78:36 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, wakisema uongo kwa ndimi zao,

Psalms 78:36 in English

Psalms 78:36 · Berean Standard Bible

But they deceived Him with their mouths, and lied to Him with their tongues.

Context

34Kila mara Mungu alipowaua baadhi yao, waliosalia walimtafuta, walimgeukia tena kwa shauku. 35Walikumbuka kwamba Mungu alikuwa Mwamba wao, kwamba Mungu Aliye Juu Sana alikuwa Mkombozi wao. 36Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, wakisema uongo kwa ndimi zao, 37mioyo yao haikuwa thabiti kwake, wala hawakuwa waaminifu katika agano lake. 38Hata hivyo alikuwa na huruma, alisamehe maovu yao na hakuwaangamiza. Mara kwa mara alizuia hasira yake, wala hakuchochea ghadhabu yake yote.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.