Native Bible

Psalms 71:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee Bwana Mwenyezi, tegemeo langu tangu ujana wangu.

Psalms 71:5 in English

Psalms 71:5 · Berean Standard Bible

For You are my hope, O Lord GOD, my confidence from my youth.

Context

3Uwe kwangu mwamba wa kimbilio, mahali nitakapokimbilia kila wakati; toa amri ya kuniokoa, kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu. 4Ee Mungu wangu uniokoe kutoka kwenye mkono wa mwovu, kutoka kwenye makucha ya watu wabaya na wakatili. 5Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee Bwana Mwenyezi, tegemeo langu tangu ujana wangu. 6Tangu kuzaliwa nimekutegemea wewe, ulinitoa tumboni mwa mama yangu. Nitakusifu wewe daima. 7Nimekuwa kama kioja kwa wengi, lakini wewe ni kimbilio langu imara.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.